fbpx
MENU

TANZANIA

T: +255 222 162 930

KENYA

T: +254 717 511 879

Plastabodi ya Knauf ni ipi?

Plastabodi ni kifaa cha ujenzi kinachotumika kujenga kuta na dari. Inatengenezwa kwa jipsam na karatasi kwahiyo ni nyepesi na rahisi kutumia. Plastabodi zinaweza kutengenezwa kwa ajili ya matumizi tofauti. Knauf inatengeneza plastabodi aina tatu: ya kawaida, yenye kudhibiti unyevunyevu na yenye kudhibiti usambaaji wa moto

Jipsam ndio kiungo kikuu kinachozipa plastabodi hizi uwezo wake. Chembechembe za jipsam zina kiasi kidogo cha maji kinachoweka plastabodi kwenye hali ya ubaridi ili kuzuia moto usisambae kwa haraka. Pia inasaidia kudhibiti kusambaa kwa sauti kwahiyo kelele haziwezi kutoka nje ya chumba husika. Kwenye makazi ya magorofani, plastabodi zinasaidia kuweka nyumba katika hali ya utulivu na ubaridi. 

Plastabodi nyingi zinakuja na chaguo la kingo za mraba au kingo zilizopigwa. Kingo za mrab hutumika kwa ajili ya kuta na dari wakati kingo zilizopigwa zinatumika kwa ajili ya miunganiko na kwa ajili ya skiming. Zinatengenezwa kwa vipimo au saizi maalum, kumaanisha kwamba plastabodi zinaweza kutumika katiza kazi mbalimbali za ujenzi bila kuhitaji kukatwa.  

Plastabodi za kawaida zina upande mmoja mweupe na upande wa pili wa rangi ya kahawia. Upande mweupe unatumika kwa ajili ya plastering na upande wa kahawia unatumika kwa ajili ya kupaka rangi au kuweka wallpaper. Plastabodi zinaweza kufungiwa kwenye fremu za chuma kwa kutumia skrubu, na hii husaidia ujenzi kufanyika kwa haraka na uwepesi zaidi. Tumia plastabodi za Knauf kwa ajili ya kazi yako ya ujenzi ili ufaidi ubora wa Kijerumani kupitia vifaa vilivyotengenezwa hapa nchini. 

___

Knauf ni kampuni inayozalisha bodi za jipsam pamoja na vifaa vyake mbali mbali Dar-es-Salaam, Tanzania. Mashine zetu ni za Kijerumani, lakini malighafi ambazo zinatumika kuzalisha jipsam zenye ubora wa juu zinapatikana  hapahapa Tanzania. Tunatengeneza jopo za plastabodi hasa kwajili ya soko la ujenzi hapa Tanzania. Tunajivunia kwa ubora wa bidhaa na huduma ambazo tunatoa kwa Watanzania.

Tuna taasisi ya utafiti na maendeleo iliyo na kiwango cha kimataifa. Lengo la taasisi yetu ni kuboresha bidhaa na uzalishaji wetu. Taasisi yetu ya utafiti imeunda mihimili inayozuia moto na unyevu, na pia tuna miundo ambayo inakubalika ki-ikolojia na vifaa vinavyostahimili tetemeko la ardhi. Suluhisho zetu za ujenzi zina hati miliki za kimataifa na zinapatikana kwa wakandarasi wote Tanzania.

Kwa maelezo zaidi juu ya bodi za plasta na vifaa vingine vya ujenzi, fuatilia kurasa zetu kwenye tovuti za Facebook na LinkedIn. Tazama sehemu yetu ya habari kwa nakala zenye maoni ya ujenzi, plastabodi na miundo ya ujenzi.

You may also enjoy