Plasterboard ni jopo nyepesi la jasi (kalsiamu sulphate dihydrate) iliyoshinikizwa kati ya karatasi mbili. Jopo hizi hutumika kutengeneza kuta na dari za ndani na kawaida huitwa drywall.
Tofauti na faida kwa upande wa bei na okoaji muda, plastabodi pia husaidia majengo kukidhi viwango vya kudhibiti moto, kelele na unyevunyevu. Knauf intengeneza aina tatu ya plastabodi; ya kawaida, ya kinga moto na ya kinga unyevunyevu. Bidhaa hizi huacha finishing safi kabisa kwenye kuta na dari na zinaweza kupakwa rangi au plasta.
Uwekaji wa plastabodi ni rahisi na huwezesha wajenzi kutengeneza kuta na dari za kawaida au zenye kupinda. Pia, plastabodi ni rafiki kwa mazingira. Zinaweza kurejeshwa tena kwa 100%, tukimaanisha kwamba- baada ya matumizi, zinaweza kusagwa tena na kuundwa upya kwa ajili ya shughuli za ujenzi.
Bidhaa hizi zitawezesha wakandarasi kujenga hospitali, shule, nyumba na sehemu za umma kwa muda mchache zaidi na kwa bei nafuu. Hii husaidia ujenzi kutokua na gharama kubwa na huhakikisha ujenzi huisha kwa muda uliopangwa. Tumia plastabodi za Knauf kwa ajili ya kazi za ujenzi zijazo na ufaidi ubora wa Kijerumani kupitia vifaa vinavyopatikana nchini.
___
Knauf ni kampuni inayozalisha bodi za jipsam pamoja na vifaa vyake mbali mbali Dar-es-Salaam, Tanzania. Mashine zetu ni za Kijerumani, lakini malighafi ambazo zinatumika kuzalisha jipsam zenye ubora wa juu zinapatikana hapahapa Tanzania. Tunatengeneza jopo za plastabodi hasa kwajili ya soko la ujenzi hapa Tanzania. Tunajivunia kwa ubora wa bidhaa na huduma ambazo tunatoa kwa Watanzania.
Tuna taasisi ya utafiti na maendeleo iliyo na kiwango cha kimataifa. Lengo la taasisi yetu ni kuboresha bidhaa na uzalishaji wetu. Taasisi yetu ya utafiti imeunda mihimili inayozuia moto na unyevu, na pia tuna miundo ambayo inakubalika ki-ikolojia na vifaa vinavyostahimili tetemeko la ardhi. Suluhisho zetu za ujenzi zina hati miliki za kimataifa na zinapatikana kwa wakandarasi wote Tanzania.
Kwa maelezo zaidi juu ya bodi za plasta na vifaa vingine vya ujenzi, fuatilia kurasa zetu kwenye tovuti za Facebook na LinkedIn. Tazama sehemu yetu ya habari kwa nakala zenye maoni ya ujenzi, plastabodi na miundo ya ujenzi.