Knauf ni kampuni inayozalisha bodi za jipsam pamoja na vifaa vyake mbali mbali Dar es Salaam, Tanzania. Mashine zetu ni za Kijerumani, lakini malighafi ambazo zinatumika kuzalisha jipsam zenye ubora wa juu zinapatikana hapahapa Tanzania. Tunatengeneza jopo za plastabodi hasa kwajili ya soko la ujenzi hapa Tanzania. Tunajivunia kwa ubora wa bidhaa na huduma ambazo tunatoa kwa Watanzania.
Tuna taasisi ya utafiti na maendeleo iliyokuwa na kiwango cha kimataifa ambayo ipo kwajili ya kuboresha bidhaa na uzalishaji wetu. Timu yetu ya watafiti imeunda bodi za jipsam zinazo zuia moto, unyevu, na sauti. Bodi zetu zimeundwa ki ikolojia na vina uwezo wa kustahimili tetemeko la ardhi. Suluhisho hizi za ujenzi zina hati miliki ya kimataifa na sasa zinapatikana kwa wakandarasi wote Tanzania.
Mbali na bidhaa za plasterboard, Knauf pia hutengeneza plasta za skimming, profaili za chuma na vifaa vya chuma kwajili ya ujenzi wa ukuta na dari. Tumejenga imani kwa wateja wetu kutokana na uzalishaji wa bidhaa zenye ubora wa hali ya juu. Bidhaa zetu zimetumika katika miradi mengi ya ujenzi, ikiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Nyerere Terminal 3 na Burj Khalifa – jengo linalo ongoza kwa urefu ulimwenguni. Tunazingatia kuwa wauzaji wa vifaa vya ujenzi wanaoaminika, kwasababu tunaweka uwazi kwa wateja kama kipaumbele chetu.
Tunaelewa kuwa tasnia ya ujenzi haiwezi kudumishwa au kufanyiwa maendeleo kama maliasili za nchi zinatumika vibaya. Knauf ina nia ya kuendelea kuunda vifaa vya ujenzi na kuendelea kutafuta suluhisho ambazo ni rafiki kwa mazingira na zinazokidhi viwango vya kimataifa kwenye ufanisi wa nishati, utendaji na ubora. Na pia, tunataka Watanzania waweze kununua vifaa vyetu kwa bei nafuu. Bidhaa zetu za plasterboard zina uwezo wa kurejeshwa. Unaweza wasiliana nasi kwa mahitaji yako ya plasterboard na vifaa vya ujenzi.
___
Kwa habari zaidi juu ya bodi za plasta na vifaa vingine vya ujenzi, fuatilia kurasa zetu kwenye tovuti ya Facebook na LinkedIn. Fuatilia sehemu yetu ya habari kwa nakala zenye maoni ya kwenye maswala ya ujenzi, plasterbodi na miundo ya ujenzi.