fbpx

Jinsi ya kuweka plasta inayounganisha bodi mbili ya jipsam za kuta

Jinsi ya kuweka plasta inayounganisha bodi mbili ya jipsam za kuta

Ishara nzuri ambayo inaonesha kwamba bodi yako ya jipsam ina ubora wa juu ni viungo kutoonekana kati ya bodi. Upatanishi wa bodi unatumia karibu ya theluthi moja ya muda unaotumika kukusanisha bodi za jipsam, lakini inategemeana aina ya uso na ubora unaohitajika. Mwongozo huu wa hatua kwa hatua utarahisisha mkandarasi yeyote aunde bodi za jipsam bila mistari ya ukutanishi kuonekana.

Bidhaa za Knauf na mifumo ya kufanyia finishing imeundwa mahsusi kukidhi mahitaji ya wakandarasi na kutoa matokeo bora kwenye upande wa finishing. Kwa kazi hii, utahitaji vifaa vya ujenzi, pamoja na yafuatayo:

  • Bodi za Knauf zilizotoboloewa 
  • Knauf JointBora (mchangayiko unaotumika kama gundo ya kuunganisha bodi)
  • Tepu ya kuunganisha bodi 
  • Trowel na Mwiko (Spatula)
  • Ndoo
  • Fimbo ya kuchanganya 
  • Ngazi
  • Msasa (p180 to p220)

Hatua za kuweka tepu kwenye muunganisho wa bodi

  1. Tumia tepu ya kuunganisha. Bidhaa hii imetengenezwa kwa matumizi ya kuunganisha bodi. Kata tepu yenye urefu wa kutosha ili uweze kuiweka kwanzia juu ya bodi mpaka chini. Hii hatua ni ya kutaarisha tepu ila sio kuweka kwenye bodi. 
  2. Changanya mchanganyiko wa drywall. Kawaida hii inakuhitaji uongeze poda ya mchanganyiko unaounganisha bodi (joint compund) kwenye ndoo ya maji. Acha unga huo (Knauf JointBora) kwa dakika tatu ili unyonye maji kabla ya kuyachanganya vizuri na fimbo yako. Jaza kwenye sehemu ya mstari unaokutanisha bodi mbili pamoja, na mwiko wa 15cm (spatula). Tumia mfagio mrefu kupaka mstari unaokutanisha bodi mbili kwa umakini, wakati ukihakikisha unaweka mchanganyiko huu kwa usawa kwanzia juu mpaka chini ya bodi zako ya jipsam unazotaka kuzikutanisha.
  3. Weka tepu ya Knauf katikati ya bodi mbili. Hapo hapo itashikamana bodi mbili. Hakikisha kwamba hakuna mikunjo au mapovu ya hewa kwenye tepu. Ni muhimu kupitisha mwiko kwenye kila upande wa tepu kuhakikisha kwamba mapovu yote ya hewa yametoka.
  4. Baada ya tepu kuambatiana na mchanganyiko ulioweka mara mwanza, unaweza paka koti ya pili kwenye bodi kufunika uso wa mkanda ambapo bodi mbili zinakutana. Hii itahakikisha kwamba mikutanisho ya  bodi hazionekani. Kwa mara nyingine tena, tumia kufagio na mwiko kusawazisha koti ya mchanganyiko kwenye bodi, ili kusiwe na utafauti wowote kwenye bodi.
  5. Acha bodi ikauke vizuri kwa masaa 24. Kisha, tumia koti ya tatu ya mchanganyiko wa drywall. Wakati huu, tumia mwiko pana ili kuhakikisha kuwa mchanganyiko unaenea pande zote za matabaka ya kwanza. Ikiwa kuna kingo kwenye bodi za kuta kavu, tumia mwiko kufuta mabonde na kuunda uunganisho ya koti 3 ulizoweka na bodi. Acha koti hii ikauke.
  6. Tumia msasa mzuri kwenye bodi yako ili iwe laini. Hii itaunda ukuta wa bodi usiokuwa na matuta au mistari.
  7. Paka ukuta na koti ya kwanza ya rangi. Tumia koti hii kama inavyopendekezwa na mtengenezaji wa rangi. Acha ikauke kisha ongeza koti mbili au tatu za rangi ya ukutani. Hii itahakikisha viungo visionekane na kukuacha na ukuta mzuri ulio na nguvu ya kudumu.

___

Knauf ni kampuni ya Kijerumani inayozalisha bodi za plasta za jipsam. Kampuni ya Knauf inafanya shughuli zake nchini Tanzania. Tunatumia vifaa vya uzalishaji kutoka hapa hapa Tanzania kutoa huduma na bidhaa zenye ubora wa juu kwenye tasnia ya ujenzi. Knauf anajivunia ubora wa bidhaa na huduma ambazo tunatoa kwa wateja.  

Kampuni ya Knauf ina timu ya watafiti ambao wameunda miundo ya kiikolojia, mifumo na vifaa venye viwango vya kimataifa na vifaa vinavyostahimili matetemeko ya ardhi. Suluhisho hizi za ujenzi zina hati miliki za kimataifa na sasa zinapatikana kwa wakandarasi wote Tanzania.

Kwa habari zaidi juu ya bodi ya plasta na vifaa vingine vya ujenzi, tufuatilie kwenye tovuti za Facebook na LinkedIn. Fuatilia sehemu yetu ya habari kwa nakala zenye maoni ya ubunifu kuhusu maswala ya ujenzi, plasterboard na miundo ya ujenzi.

You may also enjoy