fbpx
MENU

TANZANIA

T: +255 222 162 930

KENYA

T: +254 717 511 879

Jinsi ya kuweka plasta bodi ambazo zinazuia nyevu nyevu

Jinsi ya kuweka plasta bodi ambazo zinazuia nyevu nyevu

Sehemu muhimu kuliko zote kwenye ujenzi wa bafuni ni kuhakikisha kuwa kuta zako zina nguvu ya kutosha kwa matumizi ya kila siku. Hapa tunaongelea kuta za matofali na plasta, pamoja na paneli za plasterboard. Kampuni ya Knauf Tanzania hutengeneza bodi za plaster ambazo zinazuia maji/unyevu na zilizo na nguvu ya kutosha kuhimili maji na mvuke ambao hupita kwenye chumba kila siku.

Matumizi ya nyenzo sahihi kwanzia mwanzo wa ujenzi utahakikisha kwamba kuta zako zitadumu kwa muda mrefu bila kuwa na ukungu wala bovu. Matumizi mazuri ya nyenzo sahihi inaokoa pesa nyingi na inazuia hitaji la kazi za ukarabati zenye gharama kubwa hapo baadaye. Bodi za jipsam za kawaida hazitakiwi kuwekwa kama kuta au dari bafuni kwani zitanyonya mvuke wa maji na kuwa laini. Hakikisha kutumia paneli zinazopinga unyevu badala yake.

Jinsi ya kuweka drywall inayostahimili unyevu katika bafu lako

Hatua ya kwanza ya kusanikisha drywall ni kuhakikisha kuwa unatumia mabano sahihi ya chuma na frem zake za chuma. Knauf Tanzania hutengeneza vifaa vya chuma ambavyo vinafaa paneli zetu za drywall. Hakikisha unatumia profaili za chuma za Knauf kushikilia paneli za bodi ya jipsum mahali salama. Vipengele hivi huweka msingi thabiti kwajili y ukuta wenye nguvu.

Weka paneli za plasterboard kwenye profaili za chuma ukitumia screw ambazo hazitoi kutu. Ziba mapengo yote kati kati ya paneli kwa kutumia mikanda ya plasta inayounganisha kuta pamoja na mchanganyiko wa plasta. Piga msasa kwenye hivi viungo kwa kutumia msasa wenye ubora wa juu ili kuhakikisha finishing inakaa vizuri. Paka sealer ya drywall mara mbili kwenye uso mzima wa ukuta wa plasterboard kwajili ya kuzuia unyevu kabisa.

Ikiwa utaenda kuweka tiles kwenye kuta zako, tumia tiles nyepesi na zinazo zuia maji. Hii itahakikisha kwamba tiles hazianguki kutokana na mvuke wa maji yamoto watu wakiwa wanaoga. Vinginevyo, unaweza piga rangi kuta zako na koti zinazo zuia  maji pamoja na kupaka rangi za kuta za ndani mara mbili au tatu juu yake. Hii pia itazuia unyevu na ukungu na itazuia vijidudu kukua kwenye ukuta.

Hatua hizi rahisi zitakusaidia kujenga kuta za bafu zenye nguvu na zinazo dumu. Wakati plasterboard zinaathiriwa na uharibifu wa maji, drywall za Knauf zinazozuia maji na nyevunyevu  zimeundwa kulinda uimara kuna za bodi katika mazingira yenye unyevu. Weka vijidudu na uchafu mbali kwa kutumia vifaa vya Knauf na kupaka mipako sahihi ya sealer kwajili ya drywall kwenye nyuso za jopo kabla ya kuweka tiles au kupaka rangi kwenye ukuta. 

___

Knauf ni kampuni ya Kijerumani inayozalisha bodi za plasta za jipsam. Kampuni ya Knauf inafanya shughuli zake nchini Tanzania. Tunatumia vifaa vya uzalishaji kutoka hapa hapa Tanzania kutoa huduma na bidhaa zenye ubora wa juu kwenye tasnia ya ujenzi. Knauf anajivunia ubora wa bidhaa na huduma ambazo tunatoa kwa wateja.  

Kampuni ya Knauf ina timu ya watafiti ambao wameunda miundo ya kiikolojia, mifumo na vifaa venye viwango vya kimataifa na vifaa vinavyostahimili matetemeko ya ardhi. Suluhisho hizi za ujenzi zina hati miliki za kimataifa na sasa zinapatikana kwa wakandarasi wote Tanzania.

Kwa habari zaidi juu ya bodi ya plasta na vifaa vingine vya ujenzi, tufuatilie kwenye tovuti za Facebook na LinkedIn. Fuatilia sehemu yetu ya habari kwa nakala zenye maoni ya ubunifu kuhusu maswala ya ujenzi, plasterboard na miundo ya ujenzi.

You may also enjoy