fbpx

Jinsi ya kukarabati nyufa kwenye kuta kavu (drywall)

Bodi za Jipsum (au drywall) hazina gharama na ni rahisi kusanikisha. Bodi za Jipsam ni rahisi kurekebisha zikiharibika. Ajali hutokea, na wakati mwingine, kuta kavu huwa zinapata nyufa kutokana na kugongwa na fanicha (furniture), au milango ikibamizwa kwanguvu au wakati mwingine, inatokea kama watoto wakibamiza kuta. Kwa bahati nzuri uharibifu huu unaweza kutengenezwa haraka na vifaa vya Knauf ambavyo vinapatikana katika maduka ya vifaa vya ujenzi, vinginevyo mchanganyiko kwajili ukuta wa kawaida unaweza kupakwa wakati wa kutengeneza nyufa kwenye kuta na dari za bodi za plasta. 

Mchanganyiko ambao umekwisha changanywa, pia, unawezwa nunuliwa kwenye maduka ya ujenzi, lakini saa nyingine ni afadhali mteja anunuwe bodi ya plasta ya kawaida nzima na  kutoa plasta yenye ufa. Vinginevyo, nyufa ndogo, zinaweza kupakwa mchanganyiko wa plasta na kuzibwa kwa swala la dakika.

Kukarabati nyufa katika kuta za bodi za plasta

Nyufa ambazo zimesimama na nyufa ambazo zimelala zinaweza kuonekana kwenye pembe za madirisha na fremu za milango kwenye kuta kavu. Nyufa pia zinaweza sababishwa na uharibifu wa athari wakati wa usogezaji wa vitu vizito au kama kitu kizito kikidondokea kuta. Hatua za kurekebisha nyufa hizi kwenye ukuta kavu ni zifuatavyo:

Hatua ya 1: Anza kwa kupiga msasa eneo karibu na ufa kwa kutumia sandpaper. Tumia kifaa cha kunyonya vumbi na rangi zote (kifaa hiki kinaitwa vacuum machine). 

Hatua ya 2: Tumia kisu chembamba kwajili ya kupaka mchanganyiko (joint compound) mdogo wa plasta juu ya ufa. Subiri ikauke kisha piga msasa hadi ukuta uwe mlaini(smooth). Rudia hatua hii kwa kutumia koti ya pili kwajili ya kuongezea nguvu kwenye ukuta. 

Hatua ya 3: Paka rangi juu ya ukarabati ili usionekane. Kumbuka kuringanisha kwa uangalifu rangi uliyopaka na rangi ya kuta inaozunguka eneo uliyopafanyia ukarabati.

Ni rahisi sana! Ongea na msimamizi wako wa duka la vifaa, kuhakikisha kwamba unanunua mchanganyiko sahihi wa kuunganisha bodi za jipsam – mchanganyiko sahihi unahitaji kuendana na bodi za jipsam. Jisikie huru kuwasiliana nasi kwa mahitaji yako ya bodi za plasta na vifaa vya ujenzi vya ziada.

___

Knauf ni kampuni ya Kijerumani inayozalisha bodi za plasta za jipsam. Kampuni ya Knauf inafanya shughuli zake nchini Tanzania. Tunatumia vifaa vya uzalishaji kutoka hapa hapa Tanzania kutoa huduma na  bidhaa zenye ubora wa juu kwenye tasnia ya ujenzi. Knauf anajivunia ubora wa bidhaa na huduma ambazo tunatoa kwa wateja.  

Kampuni ya Knauf ina timu ya  watafiti ambao wameunda miundo ya kiikolojia, mifumo na vifaa venye viwango vya kimataifa na vifaa vinavyostahimili matetemeko ya ardhi. Suluhisho hizi za ujenzi zina hati miliki za kimataifa na sasa zinapatikana kwa wakandarasi wote Tanzania. 

Kwa habari zaidi juu ya bodi ya plasta na vifaa vingine vya ujenzi, tufuatilie kwenye tovuti za Facebook na LinkedIn. Fuatilia sehemu yetu ya habari kwa nakala zenye maoni ya ubunifu kuhusu maswala ya  ujenzi, plasterboard na miundo ya ujenzi.

You may also enjoy