fbpx
MENU

TANZANIA

T: +255 222 162 930

KENYA

T: +254 717 511 879

Jinsi ya kufunga kuta za bodi ya jasi kama mtaalamu

Jinsi ya kufunga kuta za bodi ya jasi kama mtaalamu

Makandarasi wa kitaalam hutumia mbinu mbali mbali wakati wa kusanikisha kuta za bodi za jipsam. Njia hizi zinaharakisha muda wa ufungaji na hufanya michakato ya kugonga, kupaka chapa na uchoraji uwe rahisi. Hapa chini ni hatua tano rahisi za kufunga bodi za drywall kama mtaalamu.

1. Juu na upande wa bodi 

Hatua ya kwanza ni kuweka alama ya sehemu ya ukuta kwa kutumia penseli kwenye sakafu na dari. Hii itahakikisha kuwa bodi zako zimenyooka na zimepangiliwa kwa usahihi. Kisha, tumia channel za Knauf ‘U’ zenye kipimo cha 52mm kwajili ya kichwa na msingi wa ukuta. Vyuma vya kushikilia jipsam vya 50mm Knauf Acoustic ‘C’ vinapaswa kutumika kwenye sehemu za milango ya fremu. Hakikisha unafunga kwenye ukuta na dari.

2. Jinsi ya kusanikisha urembo wa kuta uliokaa wima 

Weka vyuma vya 50mm Knauf Acoustic ‘C’  kushikilia kuta. Hakikisha kwamba unaacha nafasi sawa kati ya kila njia kwenye njia za juu ili kuwa na urembo uliokaa wima. Studi hizi zinapaswa kuwekwa kwa urefu wa 900mm ili ziringanie na makali ya bodi za Knauf. Hakuna haja ya kufunga chuma wakati huu kwani hii itafanyika baada ya bodi za plaster zikiwekwa sawa.

3. Vishikilizo vya bodi zilizolala kwa usawa

Kuweka urembo wa bodi vizuri juu ya uunganisho wa bodi mbili, unatakiwa kuweka vyuma au plate kwenye uso wa vyuma vya kuunganisha bodi. Inapaswa kuweka screw mbili za Knauf kwenye viunzi vyote vya uso wa chuma cha kuunganisha bodi. Hii itasaidia kuweka usawa wakati wa kuweka bodi za plaster.

4. Kukata paneli za bodi za plasta  

Paneli nyingi za plasterboard zinaweza kuwekwa kama zilivyo, bila uhitaji wa kukata. Lakini paneli zingine zinaweza kuhitaji kukatwa. Njia bora ya kupunguza paneli za plasterboard ni kuanza kukata kwenye upande wa uso wa karatasi na wembe kali unaotumika kukata bodi na ruler yenye usawa wa mita 1. Baada ya hapo, kunja bodi ili iachike. Bali, uso wa karatasi ya chini ya bodi bado hautakuwa imeachika, kwa hivyo tumia wembe wa ufundi kukata na kuchongesha sehemu ambazo karatasi ya bodi haijakatika vizuri. 

5. Weka paneli vizuri kama mtaalamu  

Paneli zote za plasterboard za Knauf zinapaswa kusanikishwa na uso wa bodi ukiangalia nje na ziwe zimesanikishwa kwenye urembo  na screw za Knauf. Anza kwenye upande mmoja wakati unaelekea kwenye upande mwingine wa patisheni. Kwanzia kichwani hadi sakafuni, kingo za bodi zinapaswa kuwekwa na Knauf sealant ya Knauf ili zibane vizuri. 

 Screw zinapaswa kubana kuta kwenye uso wa plasterboard bila kupasuka au kuvunja jipsam. Weka screws na misumari angalau sentimita moja kutoka pembezoni mwa bodi. Weka tepu kwenye miunganiko ili mistari miunganiko isionekane. 

6. Kata mashimo ya swichi za taa na vituo vya waya za umeme  

Ili kutoboa mashimo kwenye maeneo ya swichi za umeme na vizuizi vingine muhimu, unahitaji kuweka alama kwa uangalifu kwenye eneo la mashimo haya kwenye bodi. Njia ya haraka na rahisi ya kufanya hivyo ni kusugua chaki kando kando mwa vituo vya umeme na kisha kuweka bodi kama itakavyokuwa wakati wa kuweka. Bonyeza bodi dhidi ya sehem ambazo umeweka alama na chaki ili zile alama zionekane kwenye uso wa karatasi. Tumia msumeno au hacksaw kukata shimo kando ya alama za chaki. Hii inapaswa kuringana na swichi na vituo vya waya za umeme kikamilifu wakati bodi zitakapowekwa.

___

Knauf ni kampuni ya Kijerumani inayozalisha bodi za plasta za jipsam. Kampuni ya Knauf inafanya shughuli zake nchini Tanzania. Tunatumia vifaa vya uzalishaji kutoka hapa hapa Tanzania kutoa huduma na bidhaa zenye ubora wa juu kwenye tasnia ya ujenzi. Knauf anajivunia ubora wa bidhaa na huduma ambazo tunatoa kwa wateja.  

Kampuni ya Knauf ina timu ya watafiti ambao wameunda miundo ya kiikolojia, mifumo na vifaa venye viwango vya kimataifa na vifaa vinavyostahimili matetemeko ya ardhi. Suluhisho hizi za ujenzi zina hati miliki za kimataifa na sasa zinapatikana kwa wakandarasi wote Tanzania.

Kwa habari zaidi juu ya bodi ya plasta na vifaa vingine vya ujenzi, tufuatilie kwenye tovuti za Facebook na LinkedIn. Fuatilia sehemu yetu ya habari kwa nakala zenye maoni ya ubunifu kuhusu maswala ya ujenzi, plasterboard na miundo ya ujenzi.

You may also enjoy