fbpx
MENU

TANZANIA

T: +255 222 162 930

KENYA

T: +254 717 511 879

Gypsum inaweza kusindika na kutumika kwenye mbolea

Gypsum inaweza kusindika na kutumika kwenye mbolea

Knauf hutengeneza bodi za jipsam kwajili ya kuta na dari. Madini yetu ni bora kwa matumizi haya kwani ni ya bei rahisi na inaweza sindikwa tena. Bodi za Gypsum ni vifaa vya ujenzi vinavyolinda mazingira kwa kuwa na uwezo wa kuchakatwa katika bidhaa zingine, kama mbolea. Hii inamaanisha kwamba nyenzo zetu za taka zinaweza kutumika kwajili ya matumizi mengine na sio lazima yatupe kama takataka.

Hii inanufaisha sekta ya kilimo na mazingira. Uzalishaji wa chakula ulimwenguni na kukidhi mahitaji ya idadi ya watu inayokua ni vitu viwili ambavyo vinazingatiwa sana katika karne yetu ya 21. Kikawaida mbolea hutumiwa kuboresha mazao na kuongeza virutubishi kwenye mchanga. Bodi zetu zimetengenezwa na madini na kemikali tofauti, lakini jipsam inaweza tumika kama badala ya chaki. Chaki inasaidia mbolea iwe na muonekano mweupe.  

Mchakato wa kuchakata ni rahisi; bodi za jipsam za taka zinatibiwa kuondoa  uso wake wa karatasi ili kurekebisha pH ya jipsam. Halafu, chaki inapondwapondwa na kuchanganywa na nyenzo za kiwanda, kama majani ya zamani na vipande vya nyasi. Kisha hukaushwa. Vidonge vya mbolea hai huuzwa kwa wakulima na wamiliki wa nyumba wanaotafuta kuboresha mazao na bustani zao.

Kama madini ya asili, jipsam ni chanzo cha kalsiamu na sulphur ambazo zote ni muhimu kwa ukuaji wa mimea. Jipsam inaweza pia kusaidia rudisha pH ya mchanga tindikali na kutibu sumu ya aluminium. Hii inaunda mimea bora zaidi na inasaidia kuimarisha mifumo ya mizizi ya mimea. Faida nyingin, mbolea ya jipsam inasaidia kulegeza mchanga ulioumbana, ambao unakuza ufyonzwaji wa maji ardhini.  

Wakati nchi zingine na viwanda vya kuchakata vinachukulia jipsam kuwa dutu ya taka hatari, kuna mabadiliko yanayokua na kukubalika kwa bidhaa za jipsam kwenye vituo vya kuchakata. Sheria mpya zimefanya hii iwezekane na nchi nyingi zinagundua faida za kutumia jipsam iliyosindikwa kutengeneza mbolea, kuiweka nje ya taka zisizohitajika.

___

Knauf ni kampuni ya Kijerumani inayozalisha bodi za plasta za jipsam. Kampuni ya Knauf inafanya shughuli zake nchini Tanzania. Tunatumia vifaa vya uzalishaji kutoka hapa hapa Tanzania kutoa huduma na bidhaa zenye ubora wa juu kwenye tasnia ya ujenzi. Knauf anajivunia ubora wa bidhaa na huduma ambazo tunatoa kwa wateja.  

Kampuni ya Knauf ina timu ya watafiti ambao wameunda miundo ya kiikolojia, mifumo na vifaa venye viwango vya kimataifa na vifaa vinavyostahimili matetemeko ya ardhi. Suluhisho hizi za ujenzi zina hati miliki za kimataifa na sasa zinapatikana kwa wakandarasi wote Tanzania.

Kwa habari zaidi juu ya bodi ya plasta na vifaa vingine vya ujenzi, tufuatilie kwenye tovuti za Facebook na LinkedIn. Fuatilia sehemu yetu ya habari kwa nakala zenye maoni ya ubunifu kuhusu maswala ya ujenzi, plasterboard na miundo ya ujenzi.

You may also enjoy