fbpx
MENU

TANZANIA

T: +255 222 162 930

KENYA

T: +254 717 511 879

Faida za plastabodi katika ujenzi wa kuta

Faida za plastabodi katika ujenzi wa kuta

Moja kati ya bidhaa zinazotumika sana katika ujenzi wa kisasa ni plastabodi ambayo pia huitwa drywall. Kifaa hiki inatengenezwa na malighafi ya jipsam, inayopatikana hapahapa Tanzania na inazalishwa katika kiwanda cha Knauf.

Rahisi kuweka – Plastabodi ni nyepesi na rahisi kuweka kwenye majengo. Hii hupunguza hatari ya ajali kwa wajenzi na hufanya ujenzi uwe wa haraka na salama

Bei Nafuu – Plastabodi ni kifaa cha ujenzi chenye bei rahisi zaidi kwa ajili ya kuta na dari. Ni bei nafuu kuliko matofali au saruji. Ni bidhaa yenye ubora wa hali ya juu ambayo ina faida nyinginezo kama udhibiti wa kelele na moto.

Rafiki kwa mazingira – Plastabodi inaweza kutumika tena baada ya mara ya kwanza. Haina kemikalizo hatarishi na inatengeneza mazingira mazuri kwa makazi. 

Hudhibiti usaambaji wa moto – Knauf inatengeneza plastabodi inayoweza kupambana na usambazaji wa moto ili kukupa ulinzi zaidi itakapotokea tukio la janga la moto. Chembechembe za jipsam zinakuwa na maji, ambayo husaidia plastabodi kubaki kwenye hali ya ubaridi na unyevunyevu pindi inapokutana na moto. Hii husaidia kudhibiti kusambaa kwa moto na kuokuoa maisha. 

Hupambana na unyevunyevu – Knauf pia hutengeneza plastabodi inayopambana na unyevunyevu. Kifaa hiki kinafaa kutumika kwenye maeneo ya pwani, kama Dar es Salaam, ambapo joto na unyevunyevu ni mwingi na husababisha kuoza kwa mbao na vifaa vingine vya ujenzi. Plastabodi hubaki imara katika mazingira haya.

Rahisi kukarabati – Ukarabati  ni rahisi kwa vifaa vya plastabodi na dari. Kama jopo litavunjika au kupata ufa, ni rahisi kubadilisha na kuweka nyingine. Jopo za plastabodi huwa zinakuja kwa saizi maalum, kwahiyo jopo jipya litatoshea pengo lililoachwa na jopo la zamani lililovunjika. 

Hudhibiti kelele – Plastabodi ni nzuri kwa insulation. Hasa kwenye sauti. 

Hii husaidia kuweka hali ya utulivu na amani ndani ya nyumba – kwa kudhibiti kelele za nje na maeneo ya nyumba jirani. 

Faida hizi za plastabodi huifanya kuwa chaguo zuri kwa ajili ya wajenzi na wenye nyumba nchini Tanzania. Fikiria kuhusu kutumia plastabodi za Knauf kwa ajili ya jengo lako na ufaidi ubora wa Kijerumani kupitia vifaa vinavyopatikana hapahapa nchini.

___

Knauf ni kampuni inayozalisha bodi za jipsam pamoja na vifaa vyake mbali mbali Dar-es-Salaam, Tanzania. Mashine zetu ni za Kijerumani, lakini malighafi ambazo zinatumika kuzalisha jipsam zenye ubora wa juu zinapatikana  hapahapa Tanzania. Tunatengeneza jopo za plastabodi hasa kwajili ya soko la ujenzi hapa Tanzania. Tunajivunia kwa ubora wa bidhaa na huduma ambazo tunatoa kwa Watanzania.

Tuna taasisi ya utafiti na maendeleo iliyo na kiwango cha kimataifa. Lengo la taasisi yetu ni kuboresha bidhaa na uzalishaji wetu. Taasisi yetu ya utafiti imeunda mihimili inayozuia moto na unyevu, na pia tuna miundo ambayo inakubalika ki-ikolojia na vifaa vinavyostahimili tetemeko la ardhi. Suluhisho zetu za ujenzi zina hati miliki za kimataifa na zinapatikana kwa wakandarasi wote Tanzania.

Kwa maelezo zaidi juu ya bodi za plasta na vifaa vingine vya ujenzi, fuatilia kurasa zetu kwenye tovuti za Facebook na LinkedIn. Tazama sehemu yetu ya habari kwa nakala zenye maoni ya ujenzi, plastabodi na miundo ya ujenzi.

You may also enjoy