fbpx

Bodi ya jasi ya Knauf inaweza kutumika tena kwa 100%

Bodi ya jasi ya Knauf inaweza kutumika tena

Uchakataji wa vifaa na uimara imekuwa mada kubwa katika tasnia ya ujenzi. Takataka za ujezi pamoja na vifaa vingine vya taka kutoka kwenye site za ujenzi vinapaswa kutumiwa tena au kuchakatwa tena inapowezekana. Bidhaa za bodi za jasi za Knauf zina uwezo wa kuchakatwa kwa 100% kwasababu zimetengenezwa na vifaa vya asili.

Vipande vyetu vyenye rangi juu ya uso wa paneli za bodi za plasta vimetengenezwa kwa karatasi. Lakini, karatasi hizi sio nyenzo pekee inayotumiwa na Knauf ambayo ina uwezo wa kuchakatwa. Jipsam zetu halisi katika bidhaa zetu zinatengenezwa kwa kutumia mchakato ambao unatambuliwa na Wakala wa Ulinzi wa Mazingira kutoka Marekani Mashariki (EPA) kama zoezi endelevu la usimamizi bora wa vifaa.

Gypsum ya bandia inaweza kutengenezwa na kutumiwa kama mbadala wa jasi asili. Hii inamaanisha kuwa madini ya bidhaa zetu za plasterboard zinaweza kutengenezwa katika maabara badala ya kuondolewa chini ya udongo. Sehem za paneli za plasterboard ambazo haziwezi kutumika zinaweza kuchakatwa. Karatasi zinazowekwa kwenye uso za bodi zinaweza kuondolewa na kuchakatwa tena, na jipsam inaweza kuchakatwa na kutumiwa tena katika utengenezaji wa paneli mpya za drywall au kama nyongeza ya saruji na plasta.

Jasi iliyochakatwa inaweza kutumika kurejesha usawa wa pH ya mchanga au kama chombo cha kutibu maji kwajili ya kutuliza chembechembe zinazoelea. Jasi chakavu tayari hutumiwa kawajili ya kuunda paneli mpya za plasterboard. Knauf inafanya kazi kwajili ya kukuza njia mpya za kuingiza bidhaa zilizochakatwa kwenye safu yetu ya sasa. Wasiliana nasi kwa mahitaji yako ya plasterboard na vifaa vya ziada vya ujenzi.

___

Knauf ni kampuni ya Kijerumani inayozalisha bodi za plasta za jipsam. Kampuni ya Knauf inafanya shughuli zake nchini Tanzania. Tunatumia vifaa vya uzalishaji kutoka hapa hapa Tanzania kutoa huduma na bidhaa zenye ubora wa juu kwenye tasnia ya ujenzi. Knauf anajivunia ubora wa bidhaa na huduma ambazo tunatoa kwa wateja.  

Kampuni ya Knauf ina timu ya watafiti ambao wameunda miundo ya kiikolojia, mifumo na vifaa venye viwango vya kimataifa na vifaa vinavyostahimili matetemeko ya ardhi. Suluhisho hizi za ujenzi zina hati miliki za kimataifa na sasa zinapatikana kwa wakandarasi wote Tanzania. 

Kwa habari zaidi juu ya bodi ya plasta na vifaa vingine vya ujenzi, tufuatilie kwenye tovuti za Facebook na LinkedIn. Fuatilia sehemu yetu ya habari kwa nakala zenye maoni ya ubunifu kuhusu maswala ya ujenzi, plasterboard na miundo ya ujenzi.

You may also enjoy