Kuna aina nyingi za bodi za jipsam na kila moja huja katika miundo na saizi tofauti. Bodi zetu za jipsam ni hodari kwasababu zinaweza tumika katika kazi mbalimbali za ujenzi. Ni muhimu kwa wakandarasi kujua aina gani za bodi jipsam zinahitajika kutumika, kwasababu inasaidia kupunguza gharama za ujenzi lakini pia matumizi ya bodi elekezi yanategemeana na aina ya jengo. Hili swala la muhimu huboresha ubora wa bidhaa.
Bodi ya Gypsum pia inaweza kuitwa drywall, plasterboard au wallboard. Moja ya faida kuu ya bodi ya jipsam ni kwamba ni rahisi kusanikisha kwa sababu ya mfumo wa frem ya chuma inayoshikilia kuta na dari.
Bodi za jipsam za kawaida
Bidhaa hii ni ubao mweupe wenye msingi wa jipsam ambao nyuso zake za mbele na nyuma zimezungukwa na liner ya bodi. Bidhaa hii ni aina ya kawaida ya bodi ya plasta ambayo inatumika kwa mahitaji mbali mbali kwenye ujenzi, na sio kwa mahitaji maalum. Bodi za jipsam za kawaida zinatumika kujaza safu (layer) juu ya patisheni za kuta kavu, dari zilizokuwa suspended na vitengo vya ujenzi vilivyotengenezwa na lining za kuta.
Bodi hizi zinakuja katika vipimo viwili vya kawaida zenye pana nne kila moja. Pia kuna boda ambazo ncha zake zimechongwa (inajulikana kama tapered edge).
Bodi za jipsam ambazo zinazuia nyevu nyevu
Hii bidhaa inatumika kwajili ya mazingira ya nyevu nyevu au maji. Kwa mfano majengo ambayo yapo karibu na bahari huwa yanapata nyevu yevu kutoka baharini. Ndani ya hizi bodi tumeweka karatasi ya liner ya kijani ambayo inazuia maji kupenya. Mbali na bodi za jipsam za kawaida ambazo hatujaweka hii karatasi.
Hii boda ambayo inazuia maji Ina matumizi mazuri kwenye maeneo ya kufulia, jikoni na bafuni ambapo mvuke na unyevu unakuwepo mara nyingi.
Bodi zinazozuia moto
Bodi hizi zinapaswa kutumika wakati jengo linapimwa moto. Jipsam hizi zinashikilia kiasi kidogo cha maji ambacho kinatoka juu ya uso wa bodi wakati joto la moto likishika bodi. Hii inafanya bodi kuwa na unyevu, ambayo hupunguza kasi ya kuenea kwa moto. Msingi wa hii bodi umeimarishwa na glasi ya nyuzi (fibre) kwajili ya kukinga moto. Bodi hizi zinaweza wekwa jikoni, kwenye shaft za kuingiza na kutoa hewa (ventilator), na mahali popote ambayo inauhitaji wa kulindwa dhidhi ya moto. Ndani ya bodi hizi tumeweka karatasi nyekundu.
Bidhaa zote tatu za Knauf hutoa insulation kutokana na kelele za nje, kufanya ndani pawe eneo la utulivu. Plasterboard huzuia sauti, na kuzuia kelele zilizomo ndani ya chumba kuto kutoka nje. Bodi za jipsam zina nyenzo bora kwa kuta na dari za vyumba vya muziki, nyumba vya kuishi na maeneo ya burudani. Bodi za plaster za Knauf zinakidhi utunzaji wa mazingira na wakati tunazalisha bodi zetu, tumeweka viwango vikali vya kimataifa vya ufanisi wa nishati, ufikiaji, utendaji na ubora. Wasiliana nasi kwa mahitaji yako ya plasterboard na vifaa vya ujenzi.
___
Knauf ni kampuni ya Kijerumani inayozalisha bodi za plasta za jipsam. Kampuni ya Knauf inafanya shughuli zake nchini Tanzania. Tunatumia vifaa vya uzalishaji kutoka hapa hapa Tanzania kutoa huduma na bidhaa zenye ubora wa juu kwenye tasnia ya ujenzi. Knauf anajivunia ubora wa bidhaa na huduma ambazo tunatoa kwa wateja.
Kampuni ya Knauf ina timu ya watafiti ambao wameunda miundo ya kiikolojia, mifumo na vifaa venye viwango vya kimataifa na vifaa vinavyostahimili matetemeko ya ardhi. Suluhisho hizi za ujenzi zina hati miliki za kimataifa na sasa zinapatikana kwa wakandarasi wote Tanzania.
Kwa habari zaidi juu ya bodi ya plasta na vifaa vingine vya ujenzi, tufuatilie kwenye tovuti za Facebook na LinkedIn. Fuatilia sehemu yetu ya habari kwa nakala zenye maoni ya ubunifu kuhusu maswala ya ujenzi, plasterboard na miundo ya ujenzi.